Msafara wa Kabila wahusika kwenye ajali mbili za barabarani kwa wiki moja

Joseph Kabila Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Joseph Kabila

Msafara wa wa magari ya Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo DRC Joseph Kabila yamehusika kwenye ajali nyingine ya barabarani wakati huu akiwa nchini Zambia.

Ajali hiyo ilitokea wakati msafara wake ulikuwa ukielekea makao ya rais wa zamani Keneth Kaunda eneo la Lusaka East.

Gari dogo liligonga gari lililokuwa kwenye msafara wa rais ambapo vRais Kabila na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Joe Malanji walikuwa, kwenye barabara ya Leopards eneo la Woodlands.

Wote hawakujeruhiwa.

Ripoti za awali zilisema kuwa rais Edgar Lungu alikuwa kwenye gari lililopata ajali lakini zilikanwa na ikulu ya rais.

Hii ndiyo ajali ya pili ya barabarani kumkumba Kabila ndani ya wiki moja.

Wiki iliyoptangulia watu watano waliuaawa wakati lori dogo liligonga msafara wa rais nchini DRC.

Ripoti zilisema kuwa wanajeshi watatu na raia wawili waliuawa kwenye ajali hiyo na watu wengine 11 wakajeruhiwa.

Mada zinazohusiana