Alifungwa kwa kutunga mashahiri

Image caption Mohammed Al Ajami

Mahakama ya rufaa nchini Qatar imepunguza kifungo cha maisha cha mtunzi wa mashahiri aliyefungwa kutokana na kutunga mashairi ya kushawishi raia kuipinga Serikali.

Mahakama hiyo imepunguza kifungo hicho cha maisha hadi miaka 15 jela kwa Bwana Mohamed Al Ajami ambaye alitunga mashairi kusifu mapinduzi ya kiraia nchini Tunisia na kupinga utawala wa kifalme nchini Qatar pamoja na kupingana na serikali za nchi za kiarabu.

Mahakama kuu nchini Qatar itapitisha upya hukumu hiyo ya mahakama ya rufaa ndani ya siku 30,huku kitendo cha kufungwa kwa mtunzi huyo wa mashairi kikipingwa na wanaharakati wa haki za binadamu wakisema ni kuingilia uhuru wa kujieleza.