Awaokoa waathiriwa wa ubakaji DRC

Image caption Daktari Denis Mukgwe amepitia mengi katika juhudi zake kuwaokoa waathiriwa wa ubakaji DRC

Mzozo katika Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo si kati ya vikundi vyenye siasa kali, wala siyo nchi mbili adui. Huu ni mzozo ambao umesababishwa na maswala ya kiuchumi – na inawalenga kwa kuwaangamiza wanawake wa Kongo.

Vita nchini humo vilianza 1998 na viliisha rasmi mnamo mwaka 2003, lakini mapigano yameendelea mashariki, huku idadi ya wanaobakwa ikizidi kukua kila wa leo.

Waasi na wanajeshi wa serikali wote wamelaumiwa kwa kuwabaka wanaume na wanawake

Kwa ajili hii, watu wengi wamelazimishwa kukimbia makwao, wakiacha mashamba na rasilimali zao, kila kitu wanachomiliki. Mbinu hii imefanikiwa.

Denis Mukwege ni daktari anayeshughulikia afya ya wanawake nchini humo. Yeye na wenzake wamewahudumia waathiriwa 30,000 wa ubakaji kufikia leo.

Anasema: ”Nilijiuliza – ni nini haswa kilikuwa kinaendelea? Huu ulikuwa tu si uhalifu bali mikakati mahsusi. Kuna wakati ambapo watu wengi wangebakwa kwa mpigo, tena wazi mbele ya watu wengine – kijiji kizima kingebakwa usiku. Basi wanapofanya hivyo hawaumizi tu wanaowabaka bali jamii nzima inayolazimishwa kuwatizama.

Image caption Vita Mashariki mwa DRC vimewalazimisha mamia kutoroka makwao hali inayohatarisha maisha yao

Kuna wakati waliobakwa hujaza vitanda vyote 350 vya hospitali ya Denis Mukwege. Mradi huu wa daktari Mukwege unafadhiliwa na shirika la kuwahudumia watoto la Unicef na wahisani wengine.

Waathiriwa pia hutibiwa katika zahanati inayohamishwa hamishawa na ambayo pia inafadhaliwa na wahisani hao hao.

Anasema wanawake wangejipeleka hospitalini wakiwa wamebakwa, na kujeruhiwa sehemu zao nyeti au kupigwa risasi au hata kumwagiwa kemikali.

“Mnamo 2011, visa hivi vilipungua. Tukadhani kwamba msimu huu mbaya ulikuwa unafika ukingoni. Kumbe wapi kwa sababu tangu mwaka uliopita wakati vita vilianza tena, visa hivi vikaanza kuongezeka tena. Yaani ni hali ambayo inaandamana na vita,” alisema Mukwege.