Chadema
Huwezi kusikiliza tena

Mbona Chadema wanapanga maandamano Tanzania?

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza mikakati mitatu ya kupinga ukandamizaji wa haki na demokrasia unaodaiwa kufanywa na serikali ya Tanzania.

Mojawapo ya mikakati ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini humo ni kufanya maandamano na mikutano ya hadhara katika nchi nzima ya Tanzania Septemba mosi mwaka huu.

Regina Mziwanda amezungumza na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa chama hicho na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, ameanza kueleza hisia zake kuhusu hatua ya kupigwa marufuku kwa mikutano ya kisiasa.

Mada zinazohusiana